STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 30, 2014

Kaseba kurejesha Ligi ya Kick Boxing


BINGWA wa Taifa wa Ngumi za Kulipwa anayetambuliwa na PST, Japhet Kaseba 'Champion', amesema yupo katika mikakati ya kuirejesha tena ligi ya mchezo wa kick boxing aliyoianzisha siku za nyuma kabla ya kusimama.
Ligi hiyo iliyokuwa ikishirikisha mabingwa wa mikoa mbalimbali nchini ilisimama miaka miwili iliyopita baada ya Kaseba kujikita zaidi kwenye mchezo wa ndondi.
Akizungumza na MICHARAZO, bingwa huyo wa zamani wa dunia wa kick boxing alisema, ligi hiyo ilikwama awali kutokana na kukosa wadhamini na kitendo cha yeye kuelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ngumi.
Kaseba alisema kutokana na kutambua kwamba hakuna aliyejitokeza kuuendeleza mchezo huo nchini ameamua kujipanga upya ili kuirejesha ligi hiyo.
"Nipo katika mchakato wa kutaka kuirejesha tena ligi ya kick boxing ambayo ilianza kujizolea sifa kwa kukutanisha vipaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi, nahangaika kwa sasa kusaka wadhamini kabla ya kuitangaza rasmi," alisema.
Kaseba alisema mmoja wa wadhamini ambao anatarajiwa kuwavaa kuwaomba wamsaidie kurejesha ligi hiyo ni Eric Shigongo wa Global Publishers, aliyedai ni kati ya wadau wakubwa wa michezo nchini anayeamini atamsaidia.
Mkali huyo alisema anaamini akipata wadhamini itamsaidia kuongeza msisimko kwenye ligi hiyo iliyochezwa mfululizo kwa miaka mitatu kabla ya kuzimika kimya kimya.
Kabla ya kutumbukia kwenye ngumi, Kaseba ndiye aliyekuwa bingwa wa mchezo huo nchini na kufanikiwa kunyakua ubingwa wa dunia wa WKL na WCL.

No comments:

Post a Comment