USIKU
wa kuamkia leo Maafisa nchini Nigeria wametoa taarifa kuhusu mlipuko
uliotokea na kuua watu 19 katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa
hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya
dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini 6 kati
yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani pia magari sita
yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya ambao uko karibu na kituo
cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la
tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti
za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi
kujeruhiwa,Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu
lililotegwa ndani ya gari,Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema
aliona miili 20 ya watu waliouwawa.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo
lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza
mashambulizi kama hayo mjini Abuja,Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram
yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.
No comments:
Post a Comment