Uongozi
wa klabu ya Young Africans unapenda kuwajulisha wanachama wake, wapenzi
wa soka na wadau kwa ujumla kuwa taarifa za kuhama kwa wachezai wake
Didier Kavumbagu na Frank Domayo kwenda kujiunga na Azam FC
zisiwakatishe tamaa, ni mapenzi ya wachezaj wenyewe kwani
walishakubaliana na uongozi kila kitu juu ya kuendelea kuitumikia Yanga
kabla ya siku mbili hizi kuonekana wakiwa wamejiunga na wana ramba
ramba.
Yanga tayari ina wachezaji watatu wenye mikataba inayoendelea na kama
kanuni za VPL kwa wachezai wa kimataifa kuwa watatu zitatumika
wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi ndio
watakaoendelea, hivyo uongozi uliomba mwongozo kwa TFF juu ya taratibu
zitakazotumika kwa msimu ujao kabla ya kuwasainisha Kavumbagu na Twite.
Awali uongozi wa Yanga ulikuwa kwenye mazungumzo na wachezaji hao
tangu mwanzoni mwa msimu wa 2013/2014 juu ya kuongezewa muda wa mikataba
yao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga kwa ajili msimu mpya ujao
2014/2015.
Didier Kavumbagu na Mbuyu Twite ambao mikataba yao ilikuwa mwishoni
waliongea na uongozi tangu mapema mwaka jana mwezi wa Septemba juu ya
kuweka sahihi zao na kuendelea kuitumikia Yanga na kukubaliana mambo
yote ya msingi kikubwa kilichokuwa kinasubiriwa ni maamuzi ya TFF juu ya
usajili wa wachezaji wa kigeni msimu mpya wa 2014/2015 kwani Azimio la
Bagamoyo linapaswa kuanza kutekelezwa msimu huu
Uongozi wa Yanga uliandikia TFF barua mapema kuomba kupewa mwongozo
wa kanuni zitakazotumika kwenye usajli kwa wachezaji wa kimataifa kwa
msimu mpya kufuatia Azimio la Bagamoyo kuelekeza msimu huu kila timu
inapasa kuwa na wachezaji watatu wa kigeni, mpaka sasa uongozi wa Yanga
haujapata majibu juu ya utaratibu utakaotumika kwenye msimu wa Ligi Kuu
ijayo.
Hivyo makubaliano ya wachezaji Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na
uongozi wa Yanga SC yalikua yakisubira majibu ya TFF juu ya kanuni zipi
zitakazotumika kwenye usajili msimu wa 2014/2015 kwa wachezaji wa kigeni
na katika hali ya kushangaza Kavumbagu akaonekana tayari ameshasaini
kuichezea timu ya Azam FC.
Kuhusu Frank Domayo aliyeripotiwa jana kujiunga na Azam FC pia
alikuwa katika makubaliano ya kuongeza mkataa tangu mwezi Julai 2013,
alikubaliana na uongozi juu ya mambo yote ya msingi na kilichobakia
ilikuwa ni kuweka sahihi kwenye mkataba mpya, lakini Domayo alisema
hawezi kusaini mpaka siku atakapokuja mjomba wake ambaye ndie wakala
wake na ahadi hiyo iliendelea kwa muda wa mwaka mzima kabla ya jana
kusikia ameshasaini timu nyngine.
Habari hizi zimewashitua wapenzi, wanachama na washabiki wa Young
Africans lakini ukweli ni kuwa wachezaji wenyewe walishindwa kuwa
wakweli kwa viongozi na mwisho wa siku walikua na mipango yao ya
kuondoka, hivyo uongozi ulijtahid kadri ya uwezo wake lakini wachezaji
wanaonekana hawakua tayari kuendelea kuichezea Yanga SC.
Taarifa kamili kuhusu mipango ya timu kwa msimu ujao pamoja na ripoti
ya kocha mkuu Hans pamoja na benchi lake la Ufundi zitatolewa hivi
karibuni baada ya benchi la ufundi na uongozi kukaa kwa pamoja na
kuafikiana mipango ya msimu ujao.
Aidha uongozi wa Yanga SC unawaomba wanachama wake, wapenzi na
washabiki wasiwe na wasi wasi juu ya kuondoka kwa wachezaji hao kwani
Yanga bado ina nafasi wachezaji wengi wenye vipaji na itaendelea
kuboresha kikosi chake kwa kuzingatia maelekezo ya kocha mkuu Hans
katika usajli wa msimu ujao
No comments:
Post a Comment