Wenyeji Brazil watakaoanza mtihani wao leo dhidi ya Croatia |
FAINALI za Kombe la
Dunia zinatarajiwa kuanza kutimka rasmi kuanzia usiku wa leo kwa wenyeji wa michuano hiyo
Brazil itakapou
Brazil chini ya kocha Luis Fillipe Scolari na itakayokuwa ikimtegemea Neymar kulibakisha kombe hilo itakuwa na mtihani mbele ya Croatia.
Michuano hiyo itakayodumu kwa muda
wa mwezi mmoja, itashuhudia mataifa 32 yakichuana katika kugombea nafasi
ya kucheza fainali itakayofanyika Julai 13 jijini Rio de
Janeiro.
Mchezo huo wa ufunguzi utakaochezwa katika Uwanja wa
Corinthians uliopo jijini Sao Paulo utatanguliwa na sherehe fupi ambazo
zitakuwa na maonesho mbalimbali kuelezea uhalisia wa watu wa nchi hiyo
na soka.
Akihojiwa jana kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Luis Felipe
Scolari aliwaambia wapenzi wote wa soka kwamba muda umefika, wanatakiwa
kwenda pamoja kwasababu hilo ni Kombe lao la Dunia.
Pamoja na
shamrashamra za kuanza michuano hiyo, mwaka jana zaidi ya watu milioni
moja waliingia mtaani katika miji mikubwa kwa ajili ya kuandamana
kupinga kile walichokiita gharama kubwa za maandalizi ya michuano
hiyo.
Hata hivyo safari hii, rais wa Brazil Dilma Rousseff amesema
hataruhusu maandamano kwa ajili ya kufuruga michuano hiyo ambapo maelfu
ya polisi na wanajeshi wamepangwa ili kuhakikisha michuano hiyo
inakwenda vyema.
No comments:
Post a Comment