STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 12, 2014

Kajala aibuka na laana kivyake

Lamata aliyeiongoza filamu ya Kajala iitwayo Laana
BAADA ya kuzitumikia filamu za wenzake, hatimaye msanii Kajala Masanja amevunja ukimya akijiandaa kutoa kazi yake mwenyewe iitwayo 'Laana' kupitia kampuni yake ya Kay Entertainment.
Muongozaji wa filamu hiyo, Leah Richard 'Lamata' alisema filamu hiyo ipo ambayo Kajala ameiigiza akishirikiana na wasanii wengine nyota ipo hatua ya mwisho kabla ya kuachiwa mtaani, ikiwa ni kazi yake ya kwanza binafsi.
Lamata alisema mkasa wa filamu hiyo ni simulizi linaloelekea kweli juu ya mambo yanayowapata baadhi ya wanajamii kiasi cha kushindwa kuamini.
Baadhi ya wasanii walioshirikishwa katika filamu hiyo ni Salim Ahmed 'Gabo', Farida Sabu 'Mama Sonia' na wengine.
"Tupo katika maandalizi ya mwisho kutoa filamu mpya na ya kwanza binafsi ya Kajala iitwayo 'Laana' imeshirikisha wakali kadhaa na ni bonge la filamu," alisema Lamata mmoja wa waongozaji bora nchini wa filamu kwa sasa.
Kabla ya kutoa kazi binafsi, Kajala alitamba na filamu za watu wengine alizoshirikishwa zikiwamo, Jeraha la Moyo, House Boy, Vita Baridi, House Girl & Boy, Dhuluma, Shortcut, Basilisa, You Me and Him na Devil's Kingdom ya marehemu Steve Kanumba iliyomshirikisha nyota wa kimataifa, Ramsey Nouah.

No comments:

Post a Comment