STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

Mbwana Samatta aihofia Mambaz Jumapili

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,  Mbwana Samata, amesema mechi ya Jumapili dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakuwa na ushindani kwa pande zote mbili lakini amewataka Watanzania wasiwe na wasiwasi.
Samata na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu, waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi wakitokea Tunisia ambako klabu yao imeweka kambi kujiandaa na mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.
Akizungumza na gazeti hili juzi usiku kabla ya kupanda ndege kuja nchini, Samatta, alisema kuwa anaamini Taifa Stars ina nafasi nzuri ya kushinda mechi hiyo licha ya kwamba itakuwa ni ngumu na ni lazima wacheze kwa kujihadhari.
Samata alisema watahakikisha wanapata matokeo mazuri Jumapili na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
"Kwa upande wangu nimetoka katika maandalizi ya Ligi ya Klabu Bingwa, niko fiti kulipigania taifa langu, Inshaallah Allah atatia wepesi," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba na African Lyon (zamani Mbagala Market).
Jana mchana Samatta aliliambia gazeti hili wamefika nchini salama lakini wataungana na wachezaji wenzao wa Stars Ijumaa baada ya kurejea wakitokea Mbeya.
“Ndiyo tumeshafika Dar, niko pamoja na Tom," alisema mshambuliaji huyo anayependwa na mashabiki wa TP Mazembe.
Aliongeza kuwa wanaahidi watapambana na akawataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Jumapili kuishangilia timu hiyo.
Kabla ya kwenda Mbeya, Stars iliweka kambi ya wiki mbili jijini Gaborobe, Botswana kwa ajili ya kujiandaa na mechi hiyo ya Jumapili kabla ya kurudiana Agosti 3 mwaka huu mjini Maputo.
Nyota mwingine wa Stars kiungo, Mwinyi Kazimoto, anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea Qatar kujiunga na timu hiyo.
NIPASHE

No comments:

Post a Comment