STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

Hivi ndivyo mtoto wa Kajala, Majani alivyoadhimisha bethidei yake juzi


MTOTO wa muigizaji nyota wa filamu nchini, Kajala Masanja aitwaye Paula juzi
Sherehe hizo zilizohudhuriwa na nyota mbalimbali wa filamu nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Nyerere na mama wa mtoto huyo Kajala Masanja, zilifanyika kwenye shule hiyo iliyopo Sinza ambapo Paula na wageni waalikwa walijumuika pamoja kula keki, kuimba na kucheza na watoto hao kabla ya kuwakabidhi msaada wenye thamani ya Sh Milioni 2.
Msaada huuo ulijumuisha vyakula na vinywaji ambavyo watoto hao na walimu wao wakikabidhiwa ili kufurahia maisha kama watoto wengine.
Paula anayesoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Sun Rise, alisema kilichomsukuma kuisherehekea siku yake ya kuzaliwa pamoja na watoto hao wenye ulemavu wa akili akiwa anatimiza miaka 12 ni kutaka kuionyesha jamii inapaswa kutowasahau watoto hao ambao walionyesha kufurahia ujio wa wasanii hao na kuwatambua baadhi yao kwa majina.
"Miaka yote nasherehekea siku yangu nyumbani au shuleni kwetu, lakini safari hii nilimuomba mama nije kujumuikana watoto wenzangu shuleni hapa kama njia ya kuwafariji na pia kuikumbusha jamii kwamba watoto walemavu ni watoto kama watoto wengine hivyo wasitengwe bali wasaaidiwe kwa hali na mali. Kwa kweli nimejisikia faraja kubwa kuwapo hapa," alisema.
Kajala kwa upande wake alisema kama mzazi aliona ni nafasi nzuri ya kuungana na watoto hao na kutekeleza ombi la mwanae ambaye alimzaa na mtayarishaji maaruifu wa muziki wa kizazi kipya nchini, P Funky Majani.
"Mimi ni mzazi, niliona ni vyema kuwakumbuka watoto hawa na kuwaletea zawadi katika sherehe hizi na mwanangu Paula. Mara nyingi tumezoea kuwasaidia yatima, lakini kumbe kuna watoto wenye ulemavu kama hawa wanaohitaji pia msaada na kufarijiwa,"alisema.
Baadhi ya nyota waliomsindikiza Kajala na mwanae katika sherehe hizo ni Leah Richard 'Lamata', Chuchu Hans, Wastara Juma, Jennifer Kyaka 'Odama', Steve Nyerere, Mike Sangu, Quick Racka na wengine.

alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa akili wa Shule ya Msingi Sinza Maalum, huku akiitaka jamii kutowasahau watu wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment