STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

STEVE NYERERE AHIMIZA JAMII KUSAIDIA WALEMAVU

Steve Nyerere aliyesimama kulia akizungumza huku wanafunzi wa Shule ya Sinza Maalum wakimsikiliza walipowatembea shuleni hapo katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wa Kajala Masanja aitwaye Paula
Steve Nyerere alipokuwa akiwasilia shule ya Sinza Maalum
MWENYEKITI wa Bongo Movie, Steven Mengele 'Steve Nyerere' ameitaka jamii pamoja na wasanii wenzake nchini kubadili mtazamo wao katika kuisaidia jamii kwa kuwakumbuka pia watoto wenye ulemavu.
Steve Nyerere alitoa wito huo juzi wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wa Kajala Masanja aitwaye Paula iliyofanyika katika Shule Maalum Sinza inayofundisha watoto wenye ulemavu wa akili, ambako alisema pamoja na umuhimu wa kuwasaidia yatima, lakini pia makundi mengine ya watoto kama walemavu wa akili yanapaswa kuangaliwa kwa jicho la ziada.
"Unajua jamii na hata sisi wasanii tumezoea kila tukitaka kutoa misaada tunakimbilia kwenye vituo vya kulelea yatima, lakini kumbe wapo watoto wengine wahitaji kama watoto hawa ambao wameonyesha furaha na uwezo wa hali ya juu wa utambuzi tofauti na hali zao," alisema.
Nyota huyo wa kuigiza sauti za watu mashuhuri, aliwapongeza walimu wa shule hiyo ya Sinza Maalum kwa kazi kubwa na ngumu waliyonayo katika kuwatunza na kuwalea wanafunzi hao ambao walimtambua kwa haraka Steve Nyerere walipoulizwa kama kuna mtu yeyote katika msafara uliotembelea shuleni hapo na kumtaja yeye kwa kwenda kumshika mkono na kuamsha vicheko.

No comments:

Post a Comment