STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

BADO KIDOGO UMSIKIE THEA KWENYE INJILI

MUIGIZAJI nyota nchini, Ndimbangwe Misayo 'Thea' amesema yupo hatua ya mwisho kabla ya kuibukia studio kurekodi wimbo wake wa kwanza wa muziki wa Injili, fani anayopanga kujitosa jumla kwa lengo la kumtumia bwana.
Akizungumza na MICHARAZO, Thea alisema kuwa mpango wake wa kuhamia kwenye muziki wa Injili unaendelea kwa kuanza kutunga nyimbo kabla ya kuingia studio kwa ajili ya kurekodi ili mashabiki wa miondoko hiyo washuhudie kipaji kingine alichonacho.
"Nipo kwenye maandalizi ya kuanza kuimba nyimbo za Injili, kuna kazi nimeanza kuziandika na muda ukifika nitaingia studio na kuanza kutoa kazi moja baada ya nyingine, mashabiki wa muziki huo wavute subira," alisema.
Thea ambaye aling'ara kwenye michezo ya kuigiza ya kwenye luninga akiwa na kundi la Kaole Sanaa kabla ya kuhamia kwenye filamu alisema kiu yake ni kumtumikia Mungu kama alivyokuwa akiutumikia ulimwengu na hatanii katika hilo. Alisema uimbaji ni fani aliyokuwa nayo tangu udogoni kwa kuimba kanisani na kwenye kwaya ya kanisa lake kabla ya kuzamia kwenye filamu.

No comments:

Post a Comment