STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

KAJALA: SASA NIMEZALIWA UPYA BONGO MOVIE


NYOTA wa filamu nchini, Kajala Masanja amesema filamu yake mpya anayojiandaa kuingiza sokoni iitwayo 'Laana' inakuja kuthibitisha kuwa kwa sasa amezaliwa upya na yupo kikazi zaidi kuwapa burudani.
Kajala ambaye alinusurika kwenda jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili kabla ya kusaidiwa na Wema Sepetu kwa kumlipia faini ya Sh. milioni 13, alisema filamu hiyo mpya itatoka hivi karibuni kwani tayari ameishaikabidhi kwa wasambazaji.
Akizungumza na MICHARAZO, Kajala anayemiliki kampuni ya Kay Entertainment alisema baada ya misukosuko aliyokumbana nayo kwa sasa ametuliza akili kwa ajili ya kufanya kazi akianza na filamu ya 'Laana' ambayo amewashirikisha wasanii nyota nchini.
Kajala aliwataja baadhi ya wasanii walioicheza filamu hiyo ni Ahmed Salim 'Gabo', Philemon Lutwazi 'Uncle D', Mama Kawele, Mama Sonia, yeye (Kajala) na wakali wengine.
"Kwa sasa nipo kikazi zaidi na naanza hesabu na 'Laana' iliyotengenezwa na kampuni yangu ya Kay Entertainment chini ya muongozaji Leah Richard 'Lamata' na bada ya hapo natarajia kutoa 'Pishi' wakati 'Heart Attack' niliyoiandaa kabla ya misukosuko ikisubiri kwanza," alisema Kajala.
Msanii huyo alisema anaamini kazi hizo zitathibitisha kuwa anachokisema hatanii, bali ni kweli amezaliwa upya chini ya kampuni yake.

No comments:

Post a Comment