STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, July 17, 2014

Wastara Juma ana Last Decision kwa watu wa Mwanza

NYOTA wa filamu nchini, Wastara Juma, anajiandaa kuachia filamu yake mpya iitwayo 'Last Decision' ambayo ameshirikiana na 'vichwa' kadhaa vikali wa majiji ya Dar es Salaam na Mwanza.
Akizungumza na MICHARAZO, Wastara alisema filamu hiyo mpya iliyotayarishwa kupitia kampuni yake ya Wajey Films Production, kwa sasa ipo mikononi mwa wasambazaji kabla ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Wastara alisema filamu hiyo inasimulia mkasa wa kimapenzi ambao unamfanya mmoja wa wenza wawili kufanya mauaji ili kulipiza kisasi cha mpenzi wake, lakini msako wa polisi unakuja kumnasa mtu asiyehusika na kuibua kizaazaa kwa mhusika.
"Ni moja ya filamu ya kusisimua , sijisifii ila ina mafunzo mengi kwa jamii na nimeicheza mimi, Hemed Suleiman 'PHD' na wasanii wakali toka Mwanza akiwamo Rais wa Wasanii wa jijini hilo Anitha Kagemulo, Edwin na wengine ni mseto wa kuvutia," alisema.
Msanii huyo ambaye ni Mjane wa marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' alisema anaamini filamu hiyo itakapoingia mtaani mashabiki wa fani hiyo watamuunga mkono kwa kununua kazi halisi ili kumwezesha kupata nguvu ya kuzalisha fiklamu nyingine nzuri zaidi.

No comments:

Post a Comment