STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 14, 2014

Riyama aiogopa kesho ya Isike Samuel

Riyama Ally
Isike Samuel
KIMWANA anayetesa kwenye kiwanda cha filamu nchini, Riyama Ally ameendelea kuongeza idadi ya filamu alizocheza baada ya kushirikishwa katika kazi mpya iitwayo 'Naiogopa Kesho' inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
Riyama aliyewahi kutamba kwenye makundi mbalimbali na kisha kwenye michezo ya kwenye runinga kabla ya kuibukia kwenye filamu, akitajwa miongoni mwa waigizaji wa kike walioshirikishwa katika filamu nyingi nchini, 'atauza sura' katika filamu hiyo mali ya Isike Samuel.
Akizungumza na MICHARAZO, Isike alisema filamu hiyo ya 11 kuiandaa kupitia kampuni yake ya Classic Vision pamoja na Riyama pia imewashirikisha wakali kama Hemed Suleiman 'PHD', Frank Kusenha, Steve wa Maisha Plus na yeye mwenyewe (Isike).
"Najiandaa kuachia filamu yangu ya 11 iitwayo 'Naiogopa Kesho' ambayo nimeiigiza mimi na kuwashirikisha kina Riyama Ally, Hemed, Frank Kusenha na wengine. Ni bonge la filamu ambayo mtu hapaswi kuikosa kwa mafunzo yake," alisema.
Isike aliyejitosa kuigiza na kuzalisha filamu tangu akiwa kidato cha pili akiwa na umri wa miaka 16 tu, alisema anaamini kazi hiyo itafunika sokoni kama ilivyokuwa kwa filamu zake nyingine za nyuma ambazo ni; 'Ivan Tears', 'Eyes on Me', 'Identity Card', 'Lonely', 'Tulizana', 'Rudi Kaburini', 'Sad Moment', 'Mr Masumbuko', 'Two Sisters' na 'Family Apart'.

No comments:

Post a Comment