KOCHA wa timu ya taifa
ya Uingereza, Roy Hodgson amesema amefurahishwa na utulivu wa kikosi
chake wakati wakitafuta mbinu za kuifunga San Marino katika mchezo wa
kufuzu michuano ya Ulaya uliofanyika katika Uwanja wa Wembley.
Uingereza
ilikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili kabla ya kluongeza
mengine matano katika kipindi cha pili na kuwafanya kuibuka na ushindi
mnono wa mabao 5-0 katika mchezo huo.
Hudgson amesema kikosi chake
kifanya kazi ngumu kuipenya ngome ya San Marino iliyowapa usummbufu
lakini utulivu na subira kwa wachezaji wake vilifanya mchezo huo kuja
kuonekana rahisi.
Mabao ya Uingereza katika mchezo huo yalifungwa na
beki Phil Jagielka, nahodha Wayne Rooney aliyefunga kwa penati, Danny
Welbeck, Andros Townsend na bao la kujifunga wenyewe lililofungwa na
Alessandro Della Valle aliyebabatizwa na mpira uliopigwa na
Rooney.
Ushindi huo unawapeleka Uingereza kileleni mwa msimamo wa kundi E
kwa tofauti ya mabao dhidi ya Lithuania baada ya timu zote hizo
kushinda mechi zao mbili walizocheza.
No comments:
Post a Comment