STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 22, 2014

Marehemu YP kuzikwa leo Chang'ombe

10724259_1561586274078135_315827170_n
MWILI wa marehemu Yesaya Ambilikile 'YP', 28, msanii wa kundi la TMK Wanaume Family, anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Chang'ombe Maduka Mawili.
Msanii huyo alifaraiki usiku wa kuamkia jana kutokana na kusumbuiliwa na maradhi ya kifua yaliyomlaza katika Hospitali ya Temeke.
Marehemu YP aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa akiwa na msanii mwenzake Y Dash na wenzake wa TMK Wanaume kama 'Twende Zetu', 'Tufurahi', Dar Mpaka Moro na nyingine alizaliwa Novemba 10, 1986.
Mungu Ailaze Roho Yake Mahali Pema Ameen.

No comments:

Post a Comment