STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 22, 2014

Di Maria aleta Man Utd, kuivaa Chelsea

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/09/14/1410722741170_wps_53_epa04400505_Manchester_Un.jpg
Angel di Maria anayekuwa kuwa fiti tayari kuwavaa Chelsea Jumapili
KLABU ya Manchester United ina uhakika kuwa Angel Di Maria atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Chelsea pamoja na kupata majeruhi katika mchezo wa jana dhidi ya West Ham United. 
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alikuwa akisumbuliwa na maumivu katika kifundo cha mguu na kutolewa nje katika dakika ya 76 ya mchezo huo huku akionekana kuwekea barafu katika eneo hilo wakati akiwa benchi. 
Hata hivyo imedaiwa kuwa Di Maria amefanyiwa vipimo katika uwanja wa mazoezi wa United jana kwa ajili ya tahadhari lakini nyota huyo wa zamani wa Real Madrid anatarajiwa kuwa fiti katika mchezo dhidi ya Chelsea. 
Di Maria, 26 amekuwa katika kiwango bora toka atue Old Trafford ambapo tayari ameshatengeneza nafasi nne katika mechi sita huku akitengeneza nafasi ya bao alilofunga Marouane Fellaini katika mchezo wa juzi uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion.

No comments:

Post a Comment