SHIRIKISHO la Soka Tanzania
(TFF), kupitia Bodi ya Ligi limesema huenda likailima faini ya Sh 500,000 klabu ya Yanga kwa kitendo cha kususia kutumia chumba cha
kubadilishia nguo katika mchezo wao dhidi ya Simba SC uliofanyika Jumamosi
iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, alisema kuwa
wamezisikia taarifa hizo ambazo kwao siyo rasmi hivyo wanasubiri ripoti ya
mchezo huo ili kuijadili na kuitolea ufafanuzi.
Alisema kuwa sheria
zinaonyesha wazi kuwa, iwapo Yanga itabainika kufanya kitendo hicho lazima ikumbwe
na rungu hilo la faini kama sheria zinavyosema.
“Sheria zipo wazi na kama
kweli walifanya hivyo lazima waadhibiwe, kabla ya wiki hii kumalizika kamati
itakaa kuijadili ripoti ya mechi hiyo na faini ya shilingi laki tano itawakumba
iwapo tutalikuta suala hilo,” alisema Mwakibinga.
No comments:
Post a Comment