STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, October 22, 2014

Steven Gerrard afichua siri nzito

NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard amefichua siri kwamba aliwahi kuwinda na wapinzani wao wanaoumana leo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid.
Gerrard alisema alikuwa akiwinda na mabingwa hao watetezi wa Ulaya kwa siku za nyuma na kudokeza kuwa hata sasa akipata nafasi hiyo anaweza kuigomea.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 alikuwa akikaribia kujiunga na Chelsea 2005, huku Jose Mourinho akiweka pembeni kiasi cha pauni milioni £30 kabla ya wekundu hao kupata nafasi ya kucheza Ulaya na kumfanya kusalia.
Gerrard ametanabaisha kuwa miaka miwili Mourinho alimfuata alipokuwa meneja Santiago Bernabeu, lakini akasema kuwa alikataa kuondoka Anfield.
Timu hizo usiku wa leo zinakutana katika pambano kwenye uwanja wa Anfield, ambapo kocha Brendan Rodgers akitamba kupata ushindi ili kujiweka pazuri katika mbio za kusonga mbele kwenye makundi.

No comments:

Post a Comment