STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 5, 2015

Yanga yawabutua Coastal Union kwao, mkwakwani kimyaaaaa!

Cannavaro 6
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza nahodha wao Cannavaro kwa kufunga bao pekee la Yanga dhidi ya Coastal


Cannavaro akishangilia bao lake
Match Report: Coastal Union 0 – 1 Yanga, Yanga yakwea kileleni
Oyooooooooo! Cannavaro akishangilia bao lake
BAO pekee la Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' lilitosha kuwapa ushindi Yanga na kuwapeleka hadi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuizima Coastal Union kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Mkwakwani Tanga.
Yanga walipata ushindi huo katika mechi iliyojaa ufundi na ubabe ya kiporo kilicholeta mvuto wa aina yake kutokana na tambo na majigambo ya viongozi wa pande mbili kwamba kabla ya kuchezwa kwake.
Cannavaro amekuwa mhimili mkubwa wa Yanga kwa uhamasishaji wake, kujituma na kufunga mabao muhimu pale washambuliaji wa timu hiyo wanapozembea, aliweka kimiani bao hilo dakika ya 11 kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa wa beki Mbuyu Twite ulioparazwa na Simon Msuva na kuipa Yanga pointi tatu zilizowafanya wafikishe 22, moja zaidi ya mabingwa watetezi ambao hata hivyo wana mchezo mmoja pungufu zaidi ya Yanga.
Licha ya Coastal Unio kucharuka kusaka bao la kusawazisha walienda mapumziko wakiwa nyuma na hata katika kipindi cha pili hali ilikuw ahivyo hivyo, huku Yanga ikimpoteza mshambuliaji wake Amissi Tambwe aliyeumizwa wakati wa mchezo kipindi cha kwanza na kushindwa kurudi uwanjani.
Kwa kipigo hicho Simba ambayo Jumamosi hii wana mtihani mwingine dhidi ya Simba, wamesaliwa na pointi zao 17 baada ya mechi 13 na kusalia kwenye nafasi ya saba mbele ya Simba wenye pointi 16 baada ya mechi 12.
Ligi hiyo itaendelea tena wikiendi hii kw amichezo kadhaa huku pambano la Yanga na Mtibwa Sugar likiwa limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa wawakilishi wa Kombe la Shirikisho kujiandaa vema kabla ya kuvaana na BDF XI ya Botswana wiki ijayo kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment