STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 5, 2015

Tembo wa Afrika watangulia fainali, waigonga Kongo 3-1


afcon
Gervinho akijaribu kumtungua kipa wa DRC, Kidiaba
Wachezaji wa Tembo wa Ivory Coast wakishangilia ushindi wao wa kutinga fainali za Afcon 2015
TEMBO wa Ivory Coast, wamedhihirisha dhamira yao ya kutaka ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika baada ya kugawa dozi nene kwa Chui wa DR Congo kwa kuwalaza mabao 3-1 katika mechi ya Nusu Fainali na kutinga Fainali za michuano hiyo itakayochezwa Jumapili.
Kikosi cha Ivory Coast kikiongozwa na nahodha wake, Yaya Toure kilifanikiwa kutinga hatua hiyo ya fainali kwa kulipa kiasi ilichowahi kupewa na wapinzani wao wakati wa mechi za makundi za kuwania kwenda Guinea ya Ikweta kwa kulazwa nyumbani kwao mabao 4-3.
Wafungaji wa mabao ya wanafainali wa mwaka 2012 walikuwa Yaya Toure katika dakika ya 21, Gervinho aliyeongeza la pili dakika ya 41 na  Kanon aliyemaliza udhia katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 68.
Bao la kufutia machozi la Congo waliowang'oa watani zao wa jadi Congo-Brazzaville kwenye mechi ya robo fainali lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Mbokani dakika ya 24.

Kwa matokeo hayo Ivory Coast wanasubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya mabingwa mara nne Ghana dhidi ya Guinea ya Ikweta ili kuumana nao kwenye fainali ya Jumapili itakayoamua bingwa mpya wa Afrika baada ya taji kiutokuwa na mwenyewe kufuatia Nigeria waliokuwa mabingwa kukwa kwenda Afcon 2015.
DR Congo wenyewe watakuwa wakisubiri kujua wataumana na timu ipi itakayopoteza mchezo wa leo ili kumenyana naye katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayochezwa keshokutwa Februari 7.

No comments:

Post a Comment