STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 10, 2015

Chelsea kupeleka taji laao la ubingwa Thailand

http://soccerblitz.net/wp-content/uploads/2015/03/chelseaWinCapitalOneCup15_large.jpg
Chelsea walipotwaa taji lao la Kombe la Ligi (Capital One)

WAKATI leo wakiwa nyumbani kukabiliana na Liverpool, Mabingwa wapya wa England, Chelsea inatarajiwa kwenda kulitambulisha taji lao nchini Thailand.
Chelsea wamejumuisha katika ratiba yao kuwa Mei 30 wataenda jijini Bangkok, Thailand na kucheza na nyota wa soka wa Thailand. 
Chelsea ambao wamewahi kwenda kucheza mechi za kirafiki nchini Thailand mwaka 2011 na 2013, wanatarajiwa kucheza mchezo huo katika Uwanja wa Rajamangala kabla ya kupaa kuelekea Australia kuchukuana na Sydney FC Juni 2 mwaka huu. Chelsea pia watacheza michuano ya Kombe la Kimataifa nchini Marekani dhidi ya timu za New York Red Bulls, Paris Saint-Germain na Barcelona Julai. Waratibu wa mchezo huo huko Bangkok wamedai kuwa utakuwa mahsusi kuadhimisha miaka 88 ya kuzaliwa mfalme wa Thailand. Chelsea leo watakuwa kwenye uwanja wao wa Stamford Bridge kuwakaribisha vijogoo vya Anfield katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England. Mechi hiyo ni muhimu zaidi kwa Liverpool wanaowania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani, fursa hiyo imekuja baada ya Soothampton na Tottenham Hotspur kuchemsha katika mechi zao za wikiendi hii kwa kupokea vipigo.

No comments:

Post a Comment