STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, July 20, 2015

Michael Olunga aipeleka Gor Mahia robo fainali Kagame Cup

http://www.standardmedia.co.ke/images/saturday/stdrclwhqpq.jpg
Michael Olunga
http://2.bp.blogspot.com/-tdkAzgm1iGY/VaqXW6A-X-I/AAAAAAABYp8/3PZ8wFoFIWQ/s1600/IMG_3285.JPG
Olunga (kulia) alipoikimbiza Yanga katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Kagame ambapo alifunga moja kuisaidia Gor Mahia kushinda 2-1
MSHAMBULIAJI nyota wa Gor Mahia, Michael Olunga ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kunyakua kiatu cha dhahabu katika michuano ya Kombe la Kagame baada ya jioni hii kutupia mabao mawili kambani wakati timu yake ikiizamisha KMKM kwa mabao 3-1.
Olunga alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili na kuiwezesha Gor Mahia kuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza robo fainali ikitokea Kundi A kwa kukusanya pointi sita na mabao matano baada ya mechi yao ya awali kuitoa nishai Yanga kwa mabao 2-1.
Katika mechi huo wa kwanaa Olunga anayewindwa na Simba, ingawa ni ngumu kumpata kwani ana mkataba wa miaka miwili, alifunga bao moja.
Kwa kufunga mabao hayo mawili jana, imemfanya kuongoza orodha ya wafungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli matatu akimzidi kete Sallah Bilal wa Al Khartoum ambaye alikuwa akiongoza kwa mabao mawili baada ya mchana wa leo kuingoza timu yake kuilaza Telecom kwa mabao 5-0.
Mara baada ya mechi yake ya Yanga, Olunga alinukuliwa akisema kuwa amekuja Tanzania akiwa na nia moja ya kuwa Mfungaji Bora wa michuano hiyo, kitu kinachoonyesha ni kweli baada ya kufanikiwa kufunga mabao hayo mawili.
Kabla ya Olonga kufunga mabao hayo, Meddie Kagere mkali mwingine wa Gor Mahia aliifungia timu hiyo bao la mapema akimalizia pande la Olunga kabla ya KMKM kusawazisha na kwenda mapumziki timu zikiwa sare ya 1-1 mpaka kwenye dakika ya 65 Olunga alipoanza kufanya yake na kuwazamisha Wazanzibar.

No comments:

Post a Comment