STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 21, 2016

Simba mtegoni mwa maafande, Azam inakuwaje wana?

SImba
JKT Ruvu
Azam
Mabingwa Yanga
Mtibwa Sugar
 MABINGWA wa zamani wa soka nchini, Simba ipo kwenye mtego wa aina yake wakati kesho Jumapili wakishuka uwanjani kukamilisha msimu wa Ligi Kuu Bara 2015-2016 watakapovaana na maafande wa JKT Ruvu inayopigana kuepuka kushuka daraja.
Simba ipo mtegoni kwa sababu JKT inanolewa na nyota wake wa zamani, Abdallah Kibadeni ambaye anahitaji angalau sare ama ushindi ili kubakia ligi ya msimu ujao, lakini Wekundu wa Msimbazi wakihitaji ushindi ili kuvunjwa mwiko wa misimu mitatu mfululizo ikishindwa kushika nafasi ya pili.
Mara ya mwisho Simba kuingia kwenye Mbili Bora ni msimu walipotwaa taji lao la mwisho la ligi hiyo 2011-2012, tangu hapo imekuwa ikitaabika kushika angalau nafasi ya pili kutokana na Azam na Yanga kujimilikisha nafasi hizo na kupokezana kama mbio za vijiti.
Tayari imeshatetea ubingwa mapema na kesho ikiwa mjini Songea, Ruvuma itakuwa ikikamilisha ratiba tu dhidi ya Majimaji kwani haina cha kupoteza, huku ikiziachia msala Simba na Azam zitakazopigana vikumbo kuwania nafasi ya pili. Azam itakayoumana na timu nyingine inayochuana kuepuka kushuka daraja ya Mgambo JKT, ipo nafasi ya pili kwa sasa ikiwa na pointi 63, moja zaidi ya ilizonazo Simba.
Kama Simba itashinda na Azam kupoteza kwa Mgambo ina maana Simba itakamata nafasi ya pili, ila kama Azam itashinda na Simba kushinda bado Azam pia itatesa nyuma ya Yanga wakati Simba itabakia nafasi yake ya sasa ya tatu.
Mechi nyingine zitakazochezwa kesho kwa mujibu wa ratiba ya TFF ni Mtibwa Sugar kuvaana na  Mhanga wa kutaka kushuka daraja African Sports ya Tanga, huku Coastal Union iliyoshuka daraja tayari itaumana na Prisons inayowania nafasi ya nne ikienda sawa na Mtibwa.
Ratiba kamili ya mechi za kesho ipo hivi:

Mei 22, 2016 

Mbeya City vs Ndanda
Coastal Union vs Prisons
Simba vs JKT Ruvu
Toto Africans vs Stand United
Azam vs Mgambo JKT
Kagera Sugar vs Mwadui
Mtibwa Sugar vs Africans Sports
Majimaji vs Yanga


Msimamo wa Ligi Kuu Bara:
                            P  W  D  L   F    A  Pts

1. Yanga              29 22  6  1  68  18  72
2. Azam               29 18  9  2  46  23 63
3. Simba              29 19  5  5  44  15  62

4. Prisons             29 12 12 5  28  23  48
5. Mtibwa             29 13  8  8  31  21  47
6. Mwadui FC       29  11  8 10 29  27  41
7. Stand Utd        29  11  4  14 25 29  37
8. Majimaji           29   9   7  13 20 38 34
9.Mbeya City        29   9   7  13 32 34 34
10.Ndanda           29   7  13  9  28 30 34
11.Toto Africans   29   7   9 13  26 39 30
12.JKT Ruvu         29   7   8 14 29  42 29
13.Kagera Sugar   29   7  7  15 21  34 28
14.Mgambo          29   6   9  13 23  35 27

15.African Sports  29   7   5  17 13  32 26
16.Coastal Union  29   5  7   17 16  38 22

Wafungaji: 

21-Amissi Tambwe               (Yanga)
19-Hamis Kiiza                      (Simba)
17-Donald Ngoma                (Yanga)
14- Elias Maguli                      (Stand)
      Jeremiah Juma               (Prisons)
12- Kipre Tchetche                 (Azam)
10-John Bocco                       (Azam)
     Atupele Green              (Ndanda)
9-  Ibrahim Ajib                     (Simba)
     Shiva Kichuya               (Mtibwa)
     
     Simon Msuva                  (Yanga)
 8- Shomary Kapombe          (Azam)
  7- Fully Maganga            (Mgambo)
    Mbaraka Yusuf              (Kagera) 
    Mussa Kiumbu           (JKT Ruvu)
    Waziri Junior                     (Toto)
6- Danny Mrwanda         (Majimaji)
    
    Saady Kipanga          (JKT Ruvu) 
5- Said Bahanuzi               (Mtibwa)
    Samuel Kamuntu       (JKT Ruvu)
    Miraji Athuman                  (Toto)
    Jerry Tegete                 (Mwadui)
    Thabani Kamusoko         (Yanga)
    Mohammed Mkopi      (Prisons)
    Raphael Alpha                (Mbeya)
    AbdulRahman Mussa (JKT Ruvu)
    Didier Kavumbagu           (Azam)
4- Paul Nonga                       (Yanga)
    Aziz Gillah                   (Mgambo)
    Juma Abdul                      (Yanga)  
   Edward Christopher         (Toto)
3- Michael Aidan            (JKT Ruvu)
    Haruna Moshi                (Mbeya)
    Pastory Athanas              (Stand)
    Adam Miraj                    (Coastal)
    Kiggy Makassy             (Ndanda)
    Omar Mponda             (Ndanda)
    Peter Mapunda           (Majimaji)
   Danny Lyanga                 ( Simba)
   Babu Ally                        (Kagera)
   Mzamiru Yasin               (Mtibwa)
   Bryson Raphael            (Ndanda)
   Joseph Mahundi            (Mbeya)
   Deus Kaseke                  (Yanga)
   Mudathir Yahya              (Azam)
   Kelvin Sabato              (Mwadui)
2-Malimi Busungu              (Yanga)
   Ally Myovela                 (Prisons)
   Mohamed Ibrahim       (Mtibwa)
   Ally Shomary                (Mtibwa)
   Fabian Gwanse             (Mwadui)
   Jabir Aziz                      (Mwadui)
   Alex Kondo                   (Ndanda)
   Nassor Kapama             (Coastal)
   Thabit Khamis            (JKT Ruvu)
   Frank Domayo                  (Azam)
   Abslim  Chidiebele       (Coastal)   
   Hamad Mbumba            (Sports)
   Ditram Nchimbi     (Mbeya City)
   Kassim Selembe               (Stand)
   Nizar Khalfan                (Mwadui)
   Juma Mahadhi              (Coastal)
   Paul Ngway                    (Kagera)
   Farid Mussa                      (Azam) 
   Japhet Mkala                     (Toto)
   Chande Magoya         (Mgambo)
   Ally Ramadhani               (Sports)
   Salum Kabunda             (Mwadui)
   Kelvin Yondani                 (Yanga)  
   Salim Mbonde              (Mtibwa)
   Abdallah Juma              (Mbeya)
   Stamili Mbonde          (Majimaji)
   Omar Issa                        (Sports)
   Jumanne Alfadhil          (Prisons)
   Hassan Materema         (Sports)
   Frank William                (Prisons)
   Bolly Ajali Shaibu        (Mgambo) 
   Jaffar Ramadhani             (Toto)

No comments:

Post a Comment