STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 21, 2016

Yanga kundi moja na hawa Kombe la Shirikisho Afrika

Yanga -Tanzania
Al Ahli Tripoli-Libya
MO Bejaoa-Algeria
FUS Rabat-Morocco
Medeama-Ghana
TP Mazembe
 WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga Jumanne ijayo itajua hatima yake ya kuangukia kundi gani la Kombe la Shirikisho Afrika, lakini ikiwa na uhakika wa kukutana na Waarabu wa Afrika Kaskazini waliopenya pia katuka hatua ya makundi.
Ratiba na makundi ya michuano hiyo na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kupangwa Jumanne  mchana, lakini ikionekana wazi Yanga haiwezi kuwakwepa Waarabu ambao waingia watano katika hatua hiyo.
Timu zilizopenya hatua hiyo na kuangukia mikononi mwa Yanga ni ni TP Mazembe ya DR Congo, Madeama ya Ghana na Waarabu wa Etoile du Sahel ya Tunisia, FUS Rabat ya Morocco, Al Ahli Tripoli ya Libya, MO Bejaoa ya Algeria na Kawkab Marrakech pia ya Morocco.
Kwa timu zilizofuzu makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo nazo hiyo Jumatano ni pamoja na ES Setif ya Algeria, AS Vita ya DR Congo, Al Ahly ya Misri, Zamalek pia ya Misri, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Wydad Casabalanca ya Morocco, Enyimba ya Nigeria na ZESCO United ya Zambia.

No comments:

Post a Comment