Licha ya kuiongoza Man United kutinga Fainali ya FA CUP na pia kushika Nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England ambayo inawapa nafasi kuanza hatua ya makundi ya EUROPA LEAGUE msimu ujao, Van Gaal amekuwa akipondwa sana na mashabiki wa Man United na kila kukicha akitabiriwa kung’oka na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Msimu wote Van Gaal amekuwa kwenye presha kubwa akipondwa pia kwa staili ya uchezaji wa Timu yake na Majuzi alizomewa baada ya kutoa hotuba Old Trafford mwishoni mwa Mechi yao na Bournemouth ambayo ndiyo ilikuwa Mechi yao ya mwisho ya Ligi Msimu huu.
Kwa
mujibu wa Gazeti la The Sun la huko England, Makamu Mwenyekiti wa Man
United Ed Woodward sasa amekubali kumbadili Van Gaal na kumleta Jose
Mourinho ambae hana kibarua tangu Desemba alipotimuliwa na Chelsea. Lakini kutua kwa Mourinho si mwisho wa Van Gaal huko Old Trafford kwani inadaiwa Woodward pia ana nia ya kumbakiza Mdachi huyo ambae amebakiza Mwaka Mmoja katika Mkataba wake.
Van Gaal na Mourinho washawahi kufanya kazi wakiwa Barcelona wakati Van Gaal alipokuwa Kocha na Mourinho ndio alikuwa akichipukia na kuwa mmoja wa Wasaidizi wake.
Hadi
sasa Van Gaal na Mourinho ni Marafiki na Woodward anataka Van Gaal
abaki kama Mkurugenzi wa Soka na Mourinho awe ndie Meneja wa Timu. Hadi sasa hamna tamko rasmi kutoka Man United kuhusu ripoti hizi.

No comments:
Post a Comment