STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 6, 2018

Wenger apewa kibano, kisa kumkoromea refa

Kiocha Arsene Wenger akikoromeana na mwamuzi
LONDON, England
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich Jumapili iliyopita.
Kocha huyo alifanya kitendo hicho baada ya kukasirikia kitendo cha mwamuzi huyo Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia mkononi Calum Chambers.
Alimfuata Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya 1-1.
Wenger alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carabao dhidi ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment