STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 16, 2013

Machuppa aibeba Golden Bush Veterani kulipa kisasi kwa vijana


Athuman Machuppa enzi akicheza soka la kuilipwa Sweden
Kikosi cha Golden Bush Fc wakiwa na kocha wao Shija Katina (wa kwanza kulia waliosimama)
           

NYOTA wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Athuman Idd Machuppa asubuhi ya leo ameiwezesha timu ya Golden Bush Veterani kulipa kisasi kwa vijana wao wa Golden Bush Fc baada ya kuifungia mabao mawili yalioipa ushindi timu hiyo na kulipa kisasi cha kipigo walichopewa wiki mbili zilizopita.
Machuppa akionekana bado wamo, akishirikiana na wakali wengine waliowahi kutamba kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kama Steven Marashi, Majuto Komu, Wisdom Ndlovu, Said Swedi 'Pannuchi' na wengineo kama Kr Mullah, Majaliwa na nyota wa pambano hilo Onesmo Waziri 'Ticotixo' aliiwezesha Veterani kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Ushindi huo wa Veterani ulikuwa sawa na kipigo walichopewa na watoto wao hao wanaoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Kinondoni.
Machuppa aliyebatizwa jina la 'Smiling Killer' enzi akikipiga Msimbazi, alifunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza kwa mpira wa adhabu kabla ya kuongeza goli jingine akilifunga kiufundi katika kipindi cha pili.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Golden Bush Fc, Shija Katina yaaliipa uhai timu hiyo na kuwakimbiza Veterani walioanza kuchoka na hasa walipofanya mabadiliko kwa kuwaingiza Godfrey Katepa, Machotta, Wazir Mahadi 'Mandieta', Yahya Issa na Herry Morris.
Uhai huo wa Vijana hao waliobanwa katika kipindi cha kwanza licha ya kuwa na damu changa ziliwasaidia kujipatia bao lao la kufutia machozi, lililofungwa dakika moja kabla ya pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Kinesi, Ubungo kumalizika.

No comments:

Post a Comment