STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 19, 2013

Rage awashtaki waliofanya 'mapinduzi' Simba

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage

Na Boniface Wambura
UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umewapeleka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wanachama wake waliotangaza mapinduzi klabu hayo katika mkutano walioitisha juzi jijini Dar es Salaam.
Uongozi huo wa Simba chini ya Mwenyekiti wake wameamua kupelekea mashtaka hayo TFF kuonyesha kutokubaliana na maamuzi yaliyofanywa na wanachama hao waliotangaza kuung'oa uongozi wote wa Simba na kuunda kamati maalum.
TFF imethibitisha kupokea barua kutoka uongozi wa Simba ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo, TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na kanuni zilizopo.

No comments:

Post a Comment