STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 12, 2013

Azam yamalizana na wachezaji wake iliyowasimamia kwa rushwa

 
Add caption



KLABU ya soka ya Azam ambayo Jumapili inatarajiwa kuvaana na Simba, imemalizana na wachezaji wake wanne iliyokuwa imewasimamisha kwa tuhuma za Rushwa kabla ya kusafishwa na TAKUKURU.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu ya Azam, imesema wachezaji wote wanne waliosimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi yao wameripoti kambini tayari kuikabili Simba SC siku ya jumapili

Kurejea kwa wachezaji hao kunamaliza mgogoro uliokuwepo na kudumu kwa takribani miezi mitano kufuatia shutuma za rushwa ambazo zilipelekwa takukuru kuchunguzwa ili kujua ukweli na uongozi wa Azam FC unaishukuru takukuru kwa kazi nzuri ambapo imegundulika kuwa wachezaji hao hawakuhusika na hivyo kusafishwa na chombo hicho chenye mamlaka ya kuchunguza tuhuma za rushwa.
Wachezaji hao wote wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba SC ikiwa mwalimu ataona inafaa na wapo katika hali nzuri kuweza kucheza.
Mchezo huo wa jumapili ni muhimu sana kwa Azam FC kwani ikishinda itaizidi Simba SC pointi 14 huku simba ikisaliwa na michezo minne na hivyo kumaanisha kuwa Kagera Sugar atabaki kuwa mpinzani pekee wa Azam FC katika kuwania nafasi ya pili.

No comments:

Post a Comment