Wachezaji wa Azam walipokuwa wakijiandaa na mechi za Kombe la Shirikisho Afrika hivi karibuni |
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo wachezaji wengi 16 wameshindwa kuhudhuria siku ya kwanza ya mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye uwanja wao wa Chamazi, kutokana na sababu mbalimbali huku beki Said Murad akiwa hana taarifa yoyote ya udhuru uliomfanya asiwepo mazoezini.
Taarifa hiyo imesema wachezaji walianza mazoezi asubuhi ya leo ni pamoja na Malika Ndeule, Brian Umony, Jabir Aziz, Waziri Salum, Gaudence Mwaikimba, Luckson Kakolaki, Samih Haji Nuhu, Seif Abdallah Karihe, Wandwi Jackson na Ibrahim Mwaipopo
Wachezaji wengine 16 wamekosekana kutokana na kuomba ruksa kwa matatizo waliyonayo ya kifamilia wakiomba kuanza mazoezi wiki ijayo ambao ni David Mwantika aliye na matatizo ya kifamilia kama ilivyo kwa Omary Mtaki anayeuguza baba yake na Himid Mao aliyefiwa na baba yake mkubwa.
"Mchezaji pekee ambaye hakufika mazoezini na hakuna taarifa zozote juu ya kukosekana kwake ni Said Morad Mweda," taarifa hiyo inasomeka hivyo kuelezea kushindwa kujitokeza kwa beki huyo wa kati ambaye alisimamishwa na wenzake watatu kwa tuhuma za Rushwa kabla ya kusafishwa na TAKUKURU na kurejeshwa kikosi mwishoni mwa msimu uliopoita japo hakucheza hata mechi moja.
Moradi alisimamishwa na aliyekuwa nahodha, Aggrey Morris, kipa Deo Munishi na beki wa pembeni Erasto Nyoni.
No comments:
Post a Comment