Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Lena Mfalila akizungumza leo jijini Dar (picha:Audiface Jackson Blog) |
Aidha imeelezwa kuwa vyuo zaidi ya 200 nchini kote havina sifa ya kutoa mafunzo ya taaluma hiyo kwa kutokusajiliwa na TNMC.
Msajili
wa vyuo vya uuguzi na ukunga nchini Lena Mfalila alisema hadi sasa Baraza
linatambua uwepo wa vyuo 34 vinavyotoa mafunzo ya uuguzi nchini.
Mfalila alisema
ili mafunzo ya chuo yaweze kutambulika ni lazima kiwe kimesajiliwa, kiwe na
walimu wenye sifa pamoja kutumia mitaala inayotambuliwa na Baraza.
Aliwataka
wazazi na wanafunzi wote wanaohitaji kupata elimu katika vyuo mbalimbali hapa
nchini kuvichunguza kwanza kabla ya kujiunga navyo kwani wasipofanya hivyo
watakuwa wanapoteza muda wao.
“Lazima
wanaotaka kujiunga na chuo wanachotaka kusoma wahakikishe kama kimesajiliwa na baraza
chini ya sheria ya ‘Nursing and Midwifery’ ya mwaka 2010 na kuangalia mitaala yao
ya kufundishia,” alisema Mfalila.
Kwa
upande wa vyuo vinavyofundisha uuguzi, alisema Baraza limekumbana na changamoto
nyingi ikiwa ya kuibuka kwa vyuo ambavyo havitambuliki kisheria lakini
vinaendesha mafunzo kinyemela.
Aidha
alisema kutoka na malalamiko ya jamii
kuhudumiwa huduma duni ya uuguzi na ukunga zinazotolewa na watumishi wa afya ambao
wameajiriwa kutoka vyuo visivyotambulika,baraza
limetoa agizo kwa watumishi wa afya kutoa taarifa.
Ni vema kuonyesha vyuo vilivyosajiliwa ili kuepuka kutapeliwa kwa wanaohitji kujiunga na vyuo .
ReplyDelete