STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 12, 2013

Miaka 13 ya Kikosi sasa kuanzishwa Juni 21


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghEkj6It8ASp1m0W0hdhVaUWKSvzQLRN6D7aJbqHj2Mrl5a5u2jTOTOhWw_yzmlCqCnwWH_fGuqhkDknHP6Wz9iPLA-X7klsuuOtve9KuPx-zOl5HAhpRxTcdRLalVIRNUuwxZEdo8Kl8/s1600/kalla+pina.jpg
Kalapina kiongozi wa Kikosi cha Mizinga

BAADA ya msiba wa Albert Magweha 'Ngwair' kusababisha kuahirishwa kwa onyesho maalum la maadhimisho ya miaka 13 ya kundi la Kikosi cha Mizinga, sasa onyesho hilo litafanyika Juni 21, huku idadi ya burudani ikiongezeka ikiwamo kuongezwa kwa Fid Q, Stereo na Hamidu.
Kiongozi wa Kikosi, Karama Masoud 'Kalapina' alisema baada ya kumpumzisha msanii mwenzao, sasa onyesho lao la miaka 13 ya Kikosi itafanyika Juni 21 kwenye ukumbi ule ule wa Msasani Club, kwa kila shabiki kujilipia Sh 5,000 ili kuhudhuria na kuburudishwa kwa tani yao na burudani zilizopangwa.
Kalapina alisema kati ya burudani zitakazosindikiza maadhimisho hayo mbali na wasanii mbalimbali kama Afande Sele, Nikki Mbishi, mshindi wa tuzo tatu za Kili Music 2013, Kala Jeremiah, Nash Mc wa LWP na Manzese Crew, pia mkalio Fid Q, Stereo na Dodo Hamidu 'Nyandu Tozi' watakuwepo.
"Pia tumepanga kufanya maonyesho ya uchoraji, kuimba Free Style, maonyesho ya mavazi na kutoa tuzo kwa wadau wote waliosaidia Kikosi cha Mizinga kufika hapa ilipo wakiwamo wanahabari, wadhamin, mashabiki an wengineo waliokuwa bega kwa bega na Kikosi tangu lianzishwe," alisema Kalapina.
Kalapina alisema ameona ni vyema kupeleka onyesho lake Juni 21 ili kutogongana na maonyesho ya wasanii wengine ambao yatafanyika wiki hii ambayo nayo yaliahirishwa kabla ya kifo cha Ngwair yakiwa yamepangwa kufanyika siku moja ya Mei 31 katika kumbi tatu tofauti.
Maonyesho hayo ni ya miaka 13 ya Lady Jaydee na lile la MwanaFA ambayo kama ilivyokuwa awali yote yafanyika siku moja Juni 14 yaani Ijumaa kwenye kumbi tofauti jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment