STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 12, 2013

Kitale, Montanabe wambeba Yosso

Yosso katika pozi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjUX0UuRHZCjpum88LxYKRrQQH9fBvXBr0ag_0HocuumBL73z3ukSfyIUXEnGP0R-fe9rJ-i6FExclERL_nAl-9X_cknf204za2pnU8LPxlp8DDtHS8nXFG6YWbamC_rUGDjMHpekWpM3G/s1600/Kitale.jpg
Kitale katika pozi zake za 'kiteja'

MCHEKESHAJI ambaye kwa sasa ni mpiga picha wa filamu , Mussa Rashid 'Yosso' amejitosa kwenye muziki akijiandaa kuibuka na wimbo uitwao 'Mwanangu' alioimba akishirikiana na Mussa Yusuf 'Kitale' namuimbaji wa Extra Bongo, Michael Athanas 'Montanabe'.
Akizungumza na MICHARAZO, Yosso, aliyewahi kutamba na igizo la 'Sekeseke' lililorushwa na kituo cha ITV wakati akiwa na kundi la Kambarage, alisema wimbo huo umekamilika na kwa sasa anafanya mipango ya kuachia hewani ili mashabiki wake wapate uhondo.
Yosso, alisema wimbo huo upo katika miondoko mchanganyiko na ndani mwake Kitale na Montanabe wamefanya mambo makubwa katika kuunogesha ikizingatiwa hivyo ndiyo kazi yake ya kwanza na hivyo hakupenda kuanza vibaya ndiyo maana ameshirikisha wakali hao.
"Katika kukiendeleza kipaji changu cha muziki nilichokuwa nacho tangu mdogo kabla ya kujitosa kwenye uiogizaji, nimekamilisha wimbo wangu uitwao 'Mwanangu' ambao nimeimba pamoja na Montanabe wa Extra Bongo na Kitale, ni bonge la 'ngoma'," alisema.
Alisema wakati wimbo huo ukiandaliwa kuachiwa hewani, pia tayari ameshaanza kutayarisha nyimbo nyingine ili mara baada ya kufyatua video yake iwe rahisi kwake kurejea studio kuwapakulia mashabiki wake burudani zaidi.
Yosso, anayeandaa kipindi cha Vituko Show kama mpiga, alisema anaamini wimbo huo mpya utaonyesha ni jinsi gani alivyojipanga katika ulingo huo wa muziki baada ya kutamba kwenye uigizaji akipitia makundi ya Mtandao Arts, Dar Talent na Kambarage.

No comments:

Post a Comment