Madaktari wa nchini China walishangazwa kuona mtoto wa mwaka mmoja ana ujauzito.
Mtoto Kang Mengru wa nchini China alipelekwa hospitali baada ya
wazazi wake kushtushwa na hali ya tumbo lake kuzidi kuwa kubwa siku hadi
siku.
Baada ya mtoto huyo kufanyiwa kipimo cha ultrasound, madaktari waligundua kuwa
mtoto huyo wa kike alikuwa amebeba kitoto kichanga kwenye tumbo lake
ambacho kilikuwa kikiendelea kukua.
Madaktari wanaamini kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mimba ya
watoto wawili mapacha na pacha mmoja alijitokeza ndani ya tumbo la pacha
mwenzake.
Hali kama hiyo ya kichanga kuzaliwa ndani ya kichanga kingine ni
nadra sana kutokea na humtokea mwanamke mmoja katika wanawake 500,000.
Mtoto Kang atafanyiwa upasuaji kukiondoa kichanga hicho tumboni
No comments:
Post a Comment