STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, July 28, 2013

Maugo, Mwakyembe wachezea vichapo Russia

Mada maugo
Benson Mwakyembe
MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe waliondoka nchini na tambo za kufanya kweli nchini Russia wamejikuta wakiambulia vipigo toka kwa wenyeji wao waliopambana nao jana nchini humo.
Maugo yeye alikumbana na kipigo cha TKO ya raundi ya tano toka kwa Movsur Yusupov katika pambano la uzito wa Super Middle la raundi nane.
Bondia huyo mwenye maneno mengi alisalimu amri mwenyewe katika pambano hilo lililoichezwa kwenye viwanja wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva' Kaspiysk.

Naye Benson Mwakyembe alijikuta akichezea kichapo cha KO  ya raundi ya saba toka kwa Apti Ustarkhanov. Kama ilivyokuwa kwa pambano la Mtanzania mwenzake, Mwakyembe na mwenyeji wake walipigana katika uzito wa kilo 75 la raundi nane.
Mabondia hap walioondoka wakiapa kwenda kuwashikisha adabu wapinzani wao wanatarajiwa kurejea nchini kesho kutwa tayari na maandalizi ya mapambano yao mengine.
Maugo anatarajiwa kupanda ulingoni Agosti 30 dhidi ya Thomas Mashali katika moja ya mapambano yatakayosindikiza pigano kati ya Francis Cheka na Mmarekani Findley Derrick la kuwania ubingwa wa WBF litakalochezwa Diamond Jubilee.

No comments:

Post a Comment