STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 23, 2013

Golden Bush Veterani, Mwanza United kuvaana Jumapili


Kikosi cha Golden Bush
WAKALI wa soka la jijini Dar es Salaam, Golden Bush Veterani Jumapili inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Mwanza United inayoundwa na wakali wa zamani kama George Masatu.
Kwa mujibu wa msemaji wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico', pambano hilo litachezwa asubuhi kwenye uwanja wa Kines, maarufu kama St James Park.
Ticotico alisema kikosi chao kipo imara kwa ajili ya pambano hilo ambalo Mwana Utd inatarajiwa kusheheni wakali kama Masatu, Benjamin Magadula, Aaron Nyanda, George Nyanda Emmanuel Switta na wengineo.
"Baada ya kutoa vipigo kwa wapinzani wetu wengine wakifikia hatua ya kugoma kucheza nasi, Jumapili tutavaana na Mwanza United hivyo mashabiki waje waone soka la kutakata," alisema.
Ticotico alisema mashabiki wake washuhudie beki kisiki, Masatu akatavyokuwa na kazi ya kuwazuia washambuliaji hatari wa Golden Bush ambayo inaundwa na nyota wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars pamojana wakongwe wanaoendelea kucheza sasa.

No comments:

Post a Comment