Mabingwa watetezi Yanga watakaoanza kibarua dhidi ya Ashanti United iliyorejea ligi Kuu tena |
Na Boniface Wambura
PAZIA la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2013/2014 litafunguliwa kesho (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja saba tofauti ambapo mabingwa
watetezi Yanga wakianza kutetea ubingwa wao kwa kuikaribisha Ashanti
United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uwanja
wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro utakuwa mwenyeji wa mechi
kati ya Azam ya Dar es Salaam na wenyeji Mtibwa Sugar. Oljoro JKT
itaikaribisha Coastal Union kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta
Amri Abeid jijini Arusha.
Mgambo
Shooting itaoneshana kazi na JKT Ruvu ambayo hivi sasa iko chini ya
Kocha Mbwana Makata. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
wakati Rhino Rangers itakwaruzana na Simba katika Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi mjini Tabora.
Mbeya
City iliyopanda VPL msimu huu itapimana ubavu na Kagera Sugar kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku Ruvu Shooting
ikiialika Mabatini, Mlandizi timu ya Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Mzunguko
wa pili wa ligi hiyo utachezwa Agosti 28 mwaka huu. Baada ya hapo ligi
itasimama kupitisha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Gambia na
Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
VPL itaingia mzunguko wa tatu Septemba 14 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment