Sheikh Ponda akiwasili mahakamani |
Ulinzi wa kufa mtu! |
Tuktuk alilosafirishiwa Sheikh Ponda |
Sheikh Ponda akishuka kwenye gari |
Sheikh Ponda akiwa kizimbani |
Mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya kiongozi huyo wa umma wa Kiislam ni kutotii amri halali, kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi kutenda kosa.
Sheikh Ponda amefikishwa mjini Morogoro na helkopta
ya jeshi la polisi majira ya saa tano asubuhi chini ya ulinzi mkali
ambapo askari waliimarisha ulinzi kwa muda wote huku kikosi cha kutuliza
ghasia FFU wakiwa na silaha mabomu na mbwa ambapo hali hiyo
imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli zingine za kiofisi katika
ofisi zilizopo jirani na mahakama ya hakimu mkazi wakati kesi hiyo
ikiendelea.
Akisoma shataka mbele ya hakimu mkazi Richard Kabate , wakili
mkuu wa serikali kanda ya Morogoro Benard Kongola amedai kuwa shekh
Ponda anadaiwa kutenda makosa hayo matatu Agosti 10 mwaka huu majira ya
jioni katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Katika shitaka la kwanza la shekhe Ponda anadaiwa
kutotii amri halali ambapo shitaka la pili anadaiwa kutoa maneno yenye
nia ya kuharibu imani za dini kwa kutoa maneno kuwa serikali iliamua
kupeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi
kwa kuwaua na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa
Mtwara ni Waislamu.
Shitaka la tatu linalomkabili shekh Ponda ni
kushawishi na kutenda kosa ambapo anadaiwa kuwa alitoa maneno ya
ushawishi kwa kuwataka waislaam wasikubali uundwaji wa kamati za ulinzi
na usalama za misikiti kwani zinaundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa
CCM na serikali, na kama kamati hizo zitajitokeza aliwaamuru wafunge
milango na madirisha ya misikiti kuwapiga.
Upande wa mashitaka umedai kuwa upelelezi
umekamilika na kesi hiyo itasomwa tena Agosti 28 mwaka huu ambapo
mstakiwa amerudishwa rumande kwa helkopta jijini Dar es salaam.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo Sheikh Ponda
anayetetewa na mawakili wasomi Barthoromew Tarimo na Ignas Punge alikataa mashataka yote matatu na hivyo upande wa mashitaka
kupinga dhamana kwa madai kuwa sheikh Ponda anatumikia kifungo cha nje na
kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa
mengine.
No comments:
Post a Comment