STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 20, 2013

Mourinho bado amng'ang'ania Rooney


LICHA ya klabu ya Manchester United kupitia kocha wake, David Moyes kusisitiza kuwa mshambuliaji Wayne Rooney hauzwi, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho hajakata tamaa.
Kocha huyo mwenye maneno mengi amesisitiza kwamba klabu yake itaendeleza juhudi za kutaka kumsajili Wayne Rooney lakini watahakikisha kuwa wanafanya kila kitu "kimaadili" kuhusiana na suala la mshambuliaji huyo wa Manchester United .
Klabu hiyo ya London imeshuhudia ofa zao mbili kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 zikikataliwa, licha ya dhamira ya mshambuliaji huyo kuondoka Old Trafford na kutua Stamford Bridge katika kipindi hiki cha usajili.
Alipoulizwa kama Chelsea inaendelea kumfuatilia Rooney, Mourinho aliwaambia waandishi wa habari: "Tutajaribu hadi siku ya mwisho kuongeza mchezaji mpya kikosini, mshambuliaji.
"Lakini kwa sasa kila mshambuliaji ana klabu yake, kila mshambuliaji ni mali ya wenyewe, sidhani kama ni maadili kumtaja mchezaji ambaye ni mali ya klabu nyingine.
"Kama tutatuma ofa mpya tutafanya hivyo kiutaratibu sahihi. Hatuzungumzi na wachezaji, tunazungumza na klabu.
"Hatujaribu kufanya kama zifanyavyo klabu nyingine kwenda kujaribu kuwashawishi wachezaji kinamna fulani, sisi tunafuata njia sahihi na tutaendelea kujaribu hilo hadi siku ya mwisho ya usajili."
Chelsea walianza zama za pili za utawala wa Mourinho kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Hull City Tigers. Oscar na Frank Lampard walifunga magoli katika kipindi cha kwanza na kuwapa pointi tatu, na Mreno huyo aliwasifu mashabiki kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
"mapokezi yalikuwa mazuri. Nilikuwa iwe vile kwa sababu nilishacheza hapa nikiwa na Inter Milan kama mpimzani lakini ilikuwa ni babkubwa hivyo nilitarajia kurejea Chelsea ingekuwa vile," Mourinho alisema.

No comments:

Post a Comment