BONDIA mchachari wa ngumi za kulipwa nchini, Karama Nyilawila 'Captain'
ameondoka nchini kwenda Russia kwa ajili ya pambano lake la kimataifa
dhidi ya mwenyeji wake, Fedor Chudinov atakayepigana naye siku ya
Jumamosi (Agosti 24, 2013).
Nyilawila aliyepitia nchini Kenya kwa
ajili ya kuungana na wakala wake, Franklyn Imbenzi kwa ajili ya kuelekea
Russia, atapanda ulingoni kupigana na Chudinov katika pambano l;a uzito
wa kati la raundi nane litakalochezwa kwenye mji wa Vulgo Grad.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa
Tanzania (TPBO-Limited), ambayo ndiyo iliyotoa kibali kwa Nyilawila
kwenda Russia, bondia huyo aliondoka juzi Jumapili kupitia Nairobi Kenya
kabla ya kuelekea Urusi kwenye pambano hilo.
Hilo litakuwa pambano
la kwanza la kimataifa kwa Nyilawila, tangu 2010 alipomtwanga Kreshnik
Qato wa Albania na kutwaa taji la kimataifa la WBF ambalo
alikuja kuvuliwa baada ya kugoma kwenda kulitetea ili apigane kirafiki
na Francis Cheka mwaka 2012.
TPBO-Limited, limemtakia kila la heri
bondia Nyilawila ili apeperushe vyema bendera ya taifa kwa kufanya
vizuri katika pambano hilo la kimataifa litakalomrejesha tena kwenye
ramani ya mchezo huo.
No comments:
Post a Comment