STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 20, 2013

Man City, Pellegrini waanza kwa kishindo EPL wainyoa Newcastle 4-0

Dilva akifunga bao la kwanza la City kwa kichwa
KOCHA mpya wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini, ameanza kwa kishindo Ligi Kuu ya England baada ya usiku wa kuamkia leo kuiongoza timu yao kupata ushi9ndi wa kishidno mbele ya Newcastle United na kukwea kileleni.
Pellegrini aliyechukua nafasi ya Roberto Mancini, aliiwezesha klabu yake kupata ushindi wa mabao 4-0 nyumbani dhidi ya Newcastle na kuiengua Manchester United iliyokuwa ikiongoza baada ya jumamosi kushinda 4-1.
Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa David Silva na Sergio Aguero na mengine yaliyofungwa katika kipindi cha pili na Yaya Toure na Samir Nasri yalitosha kuipa City uongozi wa ligi hiyo iliyoanza rasmi mwishoni mwa wiki.
Silva alifunga bao lake katika dakika ya sita, kabla ya Aguero kuongeza la pili dakika ya 22, huku Newcastle ikimpoteza mchezaji wake Steven Taylor sekundu chache kabla ya mapumziko kwa kumchezea vibaya Aguero.
Magoli ya Toure na Nasri yalifungwa katika dakika ya 50 na 75.

No comments:

Post a Comment