STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 1, 2013

Polisi wauwa jambazi mkoani Iringa, yanasa wahamiaji haramu toka Ethiopia

MTU anayeshukiwa kuwa jambazi ameuawa na mwingine akikamatwa wakati wakivamia duka la Santino Mdesa katika kijiji cha Mkonge kilichopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Aidha wahamiaji haramu watano kutoka nchini Ethiopia wametiwa mbaroni kwa kosa la kuingia nchini kinyemelea ikiwa siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kuchimba mkwara juu ya wahamiaji haramu kuzidi kuongeza nchini.
Akizungumzia tukio hilo ujambazi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema majambazi hao walifyatua risasi hewani ambapo wananchi walipobaini uwepo wa tukio hilo la Uharifu walizingira eneo hilo ambapo majambazi walitambua mbinu hizo na kukimbia.
Aidha kamanda Mungi amesema wananchi kwa kushirikiana na askari polisi waliwakimbiza majambazi hao na baada ya kuzidiwa nguvu, majambazi walitupa bunduki aina ya SMG iliyokuwa na Lisasi 21, na kisha kutelekeza usafiri wao wa Pikipiki, huku askari wakifanikiwa kumpiga kwa risasi mguuni jambazi mmoja aliyekufa wakati akipelekwa kupata matibabu.
Mungi amesema pia Polisi wamefanikiwa kumkamata mwananchi wa kijiji cha Kitayawa katika Wilaya ya Iringa ambaye amekuwa akitengeneza Bunduki za kienyeji.
Katika tukio lingine kamanda Mungi amesema, wamewakamata wahamiaji haramu watano kutoka nchi ya Ethiopia ambao walikuwa wamejificha katika poli la mashamba ya kijiji cha Mazombe, katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, na kuwa wahamiaji hao walikuwa wanaelekea nchini Afrika Kusini.
Akithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji hao haramu, ofisa uhamiaji mkoa wa Iringa Ali Nassor amesema wahamiaji hao haramu wakiethiopi wapo chini ya ulinzi kwa hatua zaidi.

No comments:

Post a Comment