STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 1, 2013

Watu 7 wanusurika kufa ajali ya Ndege Longido

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1DmrEfl1anJUzU-aq9ZKrxtChtAM8ILw5c0EHEak7ECequsrmy29HWPXmMZNPDJXbucKkDbGvTUoWDUMGpujXOW5EwFxYaW5Hop0RhIDE_GbqWx51fQ1sCNL73rjzBO-CJLGm2Kf4fqBN/s320/Catalina+Aircraft+-+Canadian+Vickers+PBY-5A+Canso+-+G-PBYA+-+5242+NET.jpgWATU 7 wamenusurika kupoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka na maeneo ya Longido Mkoani Arusha juzi Jumanne.

Duru za Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha zimesema majira ya saa 8 za mchana katika kijiji cha Merugwayi ndege aina ya CESS iliyokuwa na namba za usajili TN/4206 ikiwa na marubani wawili ilipata ajali.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imetaja chanzo cha ajili hiyo kuwa ni upepo mkali uliosababisha ishindwe kupaa katika uwanja wa ndege wa Merugwayi umbali wa mita 120 na kuanguka.

Habari zaidi zinasema ndege hiyo iliondoka Arusha majira ya saa 2 za asubuhi kuelekea wilayani Ngorongoro na baadaye ilirudi tena Arusha ikiwa na Abiria watano ilipofika katika uwanja huo ilishuka kwa ajili ya kuchukua mgonjwa na ilipojaribu kuruka ilishindwa, na kupoteza mwelekeo.

Marubani waliokuwemo katika ndege hiyo ni Jaffer Shakir (23) na Patten Patrick (65).

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Japhet Lusingu amewataja majeruhi kuwa Nalepo MamaSita (38), Anna Laizer (21), Naninkoi Laizer (7), Benson Mukoya (28), Krizosto Malima (30).

Rubani wa ndege hiyo Jaffer Shakir ameumia  vibaya sehemu za usoni na amelazwa katika Hospitali ya Selian, Jijini Arusha kwa matibabu zaidi huku wengine wakiruhusiwa.  
 
Jaizmalaleo

No comments:

Post a Comment