STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 19, 2013

Baby Madaha alamba 'bingo' Kenya

Baby Madaha
Bosi Mpya wa Madaha, Joe Kariuki
MSHIRIKI wa zamani wa BSS, Baby Madaha amelamba 'bingo' baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili wa kufanya kazi na kampuni na Candy n Candy Records ya nchini Kenya wenye thamani ya Sh. Mil 20 za Kenya ambazo ni sawa na Sh. Mil 50 za kitanzania.
Mbali na donge hilo, pia kampuni hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi wake, Joe Kariuki imepa msanii huyo anayetamba kwenye fani ya muziki na filamu nchini, gari aina ya Audi TT.
Akizungumza na MICHARAZO, Baby alisema mkataba huo aliingia hivi karibuni na kampuni hiyo na tayari ameshafyatua kazi mpya kupitia kampuni hiyo iitwao 'Summer Holiday' ambao anatarajia kuizindua rasmi Oktoba 6 jijini Dar es Salaam.
Baby alisema uzinduzi huo utakaoambatana na 'party' ya kusherehekea mafanikio yake kisanii itafanyika kwenye ukumbi wa Dar Live na kusindikizwa na burudani za wasanii mbalimbali.
"Nimeingia mkataba wa miaka miwili wa kufanya kazi nchini Kenya kupitia kampuni ya Candy n Candy ambayo mbali na fedha pia wamenipa usafiri na tayari nimeshatoa kazi chini yao  iitwayo Summer Holiday iliyoanza kutamba kwenye vituo vya Channel O na MTV," alisema.
Msanii huyo aliyeibuliwa na shindano la BSS 2008, alisema anajisikia fahari kuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kupata mkataba mnono kama huo nchini Kenya na imani yake ni mwanzo wa safari yake kuelekea kwenye kilele cha mafanikio kimuziki.

No comments:

Post a Comment