WATOTO watatu wa familia moja wenye umri kati ya miaka miwili na sita, mmoja wao mwanafunzi wa shule ya awali, wamekufa baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto.
Tukio hilo lililozua simanzi kubwa, lilitokea katika Kijiji cha Lushamba, Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, saa 5:00 usiku wa kuamkia Septemba 16, mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Careen Yunus, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ingawa hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi.
Mama mzazi wa watoto hao anadaiwa kuwaacha watoto hao na kwenda kwa rafiki yake, ambaye mahusiano yao hayakutajwa.
Kitendo hicho ambacho kiliwaudhi wanakijiji na kutaka kumvamia, kumshambulia na kumuua mama huyo.
Hata hivyo, mama huyo alinusurika baada ya uongozi wa kata hiyo chini ya Afisa Mtendaji wake, Amos Mabula, kuingilia kati na kutuliza hasira za wananchi hao.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bulyaheke, Mabula, aliwataja watoto waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Joseph Alfonce (6), mwanafunzi wa Shule ya Awali Kanyala; sofia Alfonce (4) na Ndeva Alfonce (2).
Mama wa watoto hao, Naomi Kilembi (25), anashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Mumewe, Alfonce Budanda, ambaye walijaliwa kuzaa watoto wanne, akiwamo mwenye umri wa miezi mitano aliyekuwa ametoka na mama yake usiku huo, wakati tukio hilo linatokea alikuwa safarini.
Mabula alisema akiwa mlinzi wa amani katika kata hiyo, baada ya wananchi kukusanyika eneo la tukio wakiwa na hasira, mama wa watoto hao alitokea, huku watoto wakiwa wameshateketea kwa moto.
Alisema kuwa alichukua hatua baada ya mama huyo kukiri mbele yake kuwa alikuwa ametoka usiku na kuwaacha watoto hao.
Awali, Diwani wa Kata hiyo, Bagesi Ngele, akizungumzia tukio hilo, alisema tabia hiyo haiwezi kuruhusiwa kuendelea.
Alisema tukio hilo lingeweza kuzuilika kama hatua zingechukuliwa kunzia kwa familia yenyewe kwani kitendo cha kuwaacha watoto peke yao huku kukiwa moto ni cha hatari ikizingatiwa ilikuwa nyumba
No comments:
Post a Comment