STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 19, 2013

Barafu, Mzee Majuto waja na Daladala pamoja na Monalisa

Kava la filamu mpya ya msanii Barafu
Barafu
BAADA ya kuwatumikia wenzake kwa muda mrefu, hatimaye msanii mahiri wa filamu, Seleman Abdallah 'Barafu' ameibuka na kazi yake binafsi iitwayo 'Daladala' inayozungumzia mikasa, vituko na kero zote zilizopo ndani ya usafiri huo wa umma.
Ndani ya filamu hiyo, mkali huyo ameigiza na wasanii wakongwe nchini kama Amri Athuman 'King Majuto', Yvonne Cherly 'Monalisa' na wengine.
Akizungumza na MICHARAZO Barafu anayefahamika pia kama 'Mzee wa Land Rover', alisema hiyo ni kazi ya kwanza kwake kuuitoa kupitia kampuni yake iitwayo 'Mtafuna Films Production' na ni 'serious comedy'.
Barafu alisema, anatarajiwa kuitoa hadharani filamu hiyo wiki mbili zijazo, na kuwataka mashabiki kujiandaa kupata burudani na 'kuvunjika mbavu' kwa namna walivyoiigiza filamu hiyo na hasa vimbwanga vya Mzee Majuto.
"Kwa wale ambao wavijua vituko vya Mzee Majuto wajiandae kuumia zaidi kwa namna mzee huyo, mimi na Monalisa tulivyofanya mambo makubwa katika filamu hii ya 'Daladala'," alisema.
Barafu alisema baada ya kutoka kwa 'Daladala' ataanza maandalizi ya kazi zake nyingine kupitia kampuni yake mbali na zile za kushirikishwa na wenzake ambazo alidai hawezi kuziacha.

No comments:

Post a Comment