Kocha wa Azam na wasaidizi wake inatakiwa mikataba yao TFF |
Brandts wa Yanga na Minziro nao wanatakiwa mikataba yao itue TFF |
SHIRIKISHO
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha
mikataba ya makocha wao.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba 12 mwaka
huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya
ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa
kuanzia Septemba 17 mwaka huu.
Kwa
klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na vielelezo vingine
ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.
No comments:
Post a Comment