Messi akishangilia moja ya mabao yake usiku wa kuamkia leo |
Sulley Muntari akishangilia bao la ushindi la Ac Milan alilofunga lala salama |
Basel wakijipatia bao la pili lililoizamisha Chelsea 'darajani' huku Mourhino akipewa ujumbe kupitia mabango kwamba Mata atatakiwa awe uwanjani na siyo kwenye benchi. |
WAKATI Jose Mourinho na vijana wake wa Chelsea wakianguka 'darajani' kwa kulala mabao 2-1 mbele ya Basel ya Uswisi, Lionel Messi ameendelea kuboresha rekodi yake ya mabao baada ya kufunga 'hat trick' wakati Barcelona ikiizamisha Ajaz kwa mabao 4-0.
Chelsea ilikumbana na kipigo hicho na kuifanya icheze mechi nne bila kupata ushindi, japo walianza kutangulia katika mechi hiyo iliyochezwa Stanford Bridge kupata bao kupitia Oscar kabla ya Basel kusawazisha mabao yote katika kipindi cha pili.
Mabao ya washindi hao ambao wamekuwa wakizisumbua timu kubwa kila mara katika michuano hiyo, yalifungwa na Salah dakika ya 71 na Streller dakika ya 82.
Katika mechi nyingine Barcelona ikiwa uwanja wake wa nyumbani iliisasambua Ajax ya Uholanzi kwa kuishindilia mabao 4-0, huku 'mchawi mweupe' Messi akitumbukiza mara tatu na kuondoka na mpira wake nyumbani.
Bao jingine la mabingwa hao wa Hispania lilifungwa na Gerard Pique, ilihali Arsenal wakiwa ugenini nchini Ufaransa walitakata baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Olympique Marseille nao Ac Milan ikiwa nyumbani ilifunga Celtic mabao 2-0.
Mecchi nyingine matokeo yake ni Schalke 04 kuilaza Steau Bucharest mabao 3-0, Napoli kuitafuna Borussia Dotmund ya Ujerumani mabao 2-1 nchini Italia, kadhaalika Atletico Madrid wakitakata nyumbani kwa kuilaza Zenit kwa mabao 3-1na Porto ya Ureno kushinda ugenini mbele ya wenyeji wa Austria Wien.
No comments:
Post a Comment