ZIKIWA zimepita siku chache toka
mmoja kati ya madereva boda boda mjini Iringa kutekwa kisha kujeruhiwa
vibaya kabla ya kuporwa pikipiki yake ,unyama huo dhidi ya madereva
boda boda umeendelea kutikisa mji wa Iringa baada kijana mmoja mkazi wa
kihodombi kutekwa kisha kuuwawa kinyama.
Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa leo baada ya kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Edger Lalika kukutwa ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani .
Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa matukio daima .com kuwa tukio la kuuwawa kwa dereva boda boda huyo liletokea eneo la Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Hata hivyo kijana huyo anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 20,ameuwa akiwa anafanya shughuli zake za bodaboda baada ya kukodiwa na mteja wake huyo ambae aliamua kuitoa roho yake kabla ya kumpokonya boda boda.
Kutokana na tukio hilo baadhi ya madereva bodaboda wamelaani vikali kitendo hicho na kuwataka madereva bodaboda wengine kuungana na kushirikiana na jeshi la polisi kufichua vitendo hivyo vya utekaji na mauwaji dhidi ya madereva boda boda.
Mazishi ya kijana huyo yanafanyika leo katika makaburi ya mlolo Iringa mjini
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limethibitisha kutokea kwa mauwaji hayo.

Matukio Daima
No comments:
Post a Comment