STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 5, 2013

Ajali nyingine tena, 15 waumia vibaya 40 wanusurika kufa basi la JM Luxury Coach

Wananchi  na kijiji  cha Mazombe  Kilolo  pamoja na abiria  wa basi la JM Luxury Coach  wakilitazama basi  hilo baada  ya  kupinduka  eneo la Mazombe  leo majira ya  saa 11 jioni wakati  likitokea  Dar  kuja  Iringa mjini basi  hilo lenye namba za usajili T 957 CGK
Basi la JM baada  ya  kupinduka
Mmoja kati ya majeruhi  wa ajali hiyo akitoka katika basi la JM baada ya ajali
Majeruhi  wa ajali ya JM akitafuta  mizigo  yake
Abiria  wakitoka katika  basi hilo baada ya kupinduka
ABIRIA  15   waliokuwa  wakisafiri  na basalaam kuelekea  mjini Iringa  wamejeruhiwa  vibaya huku  wengine  zaidi  ya 40  wakinusurika  kifo  baada  ya basi  hilo lenye namba za usajili TT 957 CGK kuacha  njia na kupinduka

Ajali  hiyo  imetokea leo majira ya saa 11  jioni katika eneo la Mazombe Ilula  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa  katika barabara kuu ya Dar es Salaam  - Iringa

Mashuhuda  waliozungumza na mtandao huu  wa www.matukiodaima.com eneo la  tukio  walidai kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva  kushindwa  kulimudu gari  hilo.

Kwani walisema  kuwa  eneo hilo lenye  kona dereva  alikuwa katika mwendo na  kuhama njia kabla ya kupinduka na kuwa katika ajali  hiyo watu  15 wamejeruhiwa vibaya na wengine  kunusurika na kuwa majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.

Jeshi la polisi mkoa  wa Iringa  limethibitisha tukio  hilo na kuwa hakuna aliyepoteza maisha katika ajali  hiyo.

No comments:

Post a Comment