STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 5, 2013

Manchester United wazinduka kwa 'vibonde'

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhe3IKQni8iK4k55YF9AJTApI9vuT9IbZfvVjGD7spIAaXFZr2VTfKKgYwShNsPIWfR9i_3phiURNMa9AF9mqCuuEBZ-RzsMgbm9H2KAcEfpG0UMS_o6ot41MkToTtpI4PTHoyugIOjtcA9/s640/Manchester+United2.jpg
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England muda mchache uliopita wamenusurika kupata kipigo kingine katika ligi hiyo baada ya kuicharaza 'vibonde' Sunderland iliyokuwa nyumbani kwao kwa mabao 2-1.
Shukrani za Mashetani Wekundu zinaenda kwa Adnan Januzaj aliyefunga mabao yote mawili ndani ya dakika moja katika kipindi cha pili na kuipa ushindi humno vijana wa David Moyes.
Wenyeji wanaoburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo waliwashtukiza Manchester kwa kupata bao la kuongoza lililofungw adakika ya tano tu ya mchezo huo na Craig Gardner na kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Hata hivyo vijana wa Moyes waliingia kipindi cha pili wakiwa wamebadilika na kujipata bao la kusawazisha dakika ya 61 wakati Januzaj akimalizia kazi nzuri ya Patrick Evra kabla ya kuongeza la pili dakika moja baadaye na kuipa ushindi Manchester United iliyotoka kudunguliwa mechi mbili mfululizo katika ligi hiyo na kulazimishwa sare ya 1-1 kwwnye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Shakhtar Donetsk katikati ya wiki.

No comments:

Post a Comment